Upendo Unaopima Mioyo ya Wengine

Tunafurahi tunapofanya jambo jema linaloweza kugusa moyo wa mtu mwingine.

Tufikirie mfano mmoja. Watoto wa mama mmoja walikusanyika kusherehekea siku yake ya kuzaliwa ya miaka sitini. Mama huyo alikuwa amefiwa na mumewe mapema katika ndoa yao, lakini kwa juhudi zake aliwalea watoto wake wote kwa mafanikio.

Ili kumshukuru kwa wema wake, kila mtoto alitayarisha zawadi bora kadiri alivyoweza. Mmoja alimpa mamia ya maelfu ya dola, wa pili akanunua tiketi za ndege kwa ajili ya safari yake ya ng’ambo, na wa tatu akamletea chakula kizuri na chenye afya. Mtoto wa mwisho akatoa bakuli la kitoweo cha kuku na kuliweka mezani. Mama alitabasamu na kuzitazama zawadi zote nne, kisha akavuta bakuli la kitoweo karibu naye na kuanza kukila kwa furaha. Watoto walishangazwa sana na kitendo chake kisichotarajiwa.

Bakuli la kitoweo cha kuku lilionekana duni sana likilinganishwa na zawadi nyingine za gharama kubwa. Watoto watatu wakubwa walidhani mama yao hangeweza kula kitoweo cha kuku kwa sababu ya mzio fulani. Hadi wakati huo alikuwa amewaambia watoto wake kwamba hangeweza kula kuku uliopikwa kwa kitoweo, lakini sababu halisi ilikuwa kwamba walipitia nyakati ngumu na alitaka watoto wale chakula hicho kwa uhuru. Ni muhimu sana kuelewa mioyo ya wengine.

Unaposhirikiana na mtu yeyote—iwe ni mzazi, ndugu, rafiki, mtu mkubwa, rika lako au mdogo—usitazame matendo yake ya nje tu; ukielewa moyo wake, unaweza kumtumikia kwa upendo wa kweli na wa hiari. Upendo huo una thamani kubwa na hugusa mioyo ya wengine. Katika Marko 10, mtu mmoja alimkimbilia Yesu na kumuuliza, “Mwalimu Mwema, nifanye nini ili niurithi uzima wa milele?” Yesu akamjibu kwa kumuuliza ikiwa alikuwa amezishika amri zilizo katika Biblia.

Mtu huyo akamwambia Yesu kwa ujasiri, “Mwalimu, hayo yote nimeyashika tangu utoto wangu.” Yesu akamtazama na kumpenda, kisha akamwambia, “Umepungukiwa na neno moja; nenda ukauze ulivyo navyo vyote, uwape maskini, nawe utakuwa na hazina mbinguni; kisha njoo, unifuate.” Aliposikia maneno hayo akahuzunika na kuondoka kwa masikitiko, tofauti na alivyokuja kwa ujasiri kumuuliza Yesu. Alionekana kuwa ameishi maisha ya kumcha Mungu, lakini moyoni alipenda mali yake na fedha kuliko Mungu. Ndiyo maana hakuweza kutii Yesu alipomwambia auze mali yake yote, awape maskini, kisha amfuate.

Alikosa nafasi tukufu ya kuwa mwanafunzi wa Yesu. Hata leo, kama yule kijana tajiri, waumini wengi husema wanaishi kulingana na mapenzi ya Mungu, lakini ni vigumu kupata wanaouelewa moyo wa Mungu, wanaotii hata inapoonekana vigumu kutii, wanaowahudumia watoto wadogo na kuwapenda watu wote walio karibu nao.

Ninaomba kila mmoja wenu atambue kwamba kuelewa mioyo ya wengine na kuwatumikia kwa ukweli na matendo kuna thamani kubwa kuliko hazina ya gharama kubwa; na kwamba awe na upendo wa kweli. Ninaomba haya katika jina la Bwana wetu!

    His Emeritus Bishop Dr. Jaerock Lee

Word of Life